Ameyasema hayo, wakati Mke wa Rais wa Finland Mama Suzanne Innes-Stubb alipomtembelea mama Maryam Mwinyi huko Migombani Wilaya ya Mjini.
Amesema, mashirikiano hayo yaliodumu kwa muda mrefu, yamepelekea kudumisha ustawi wa Maendeleo kwa nchi mbili hizo.
Amesema, ujio wa Kiongozi huyo, ni fursa muhimu kwa Tanzania kwani imekuwa na vivutio mbalimbali vya Utalii kama vile, Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar, Mlima Kilimanjaro na Mbuga za Serengeti.
Aidha amesema, matumaini yake, kuwa Kiongozi huyo, ataweza kuitangaza Taasisi ya Zanzibar Maisha bora foundation na Zanzibar kwa ujumla kutokana na kazi nzuri, inayofanywa na Taasisi hiyo.
Mbali na hayo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ina mashirikiano makubwa na Taasisi za kijamii, Taasisi za ndani na mashirika mbalimbali ya nje na ndani ya Nchi.
Amesema ,Taasisi ya Zanzibar Maisha bora foundation, ipo mstari wa mbele katika kusaidia na kuwawezesha Wananchi wa makundi mbalimbali ili kuwasaidia katika kuendesha maisha yao.
Kwa upande wake Mke wa Rais wa Finland Mama Suzanne Innes-Stubb amesema ameridhushwa na mapokezi ya Kiongozi huyo na kuahidi kushirikiana kwa maslahi ya pande zote mbili.
Aidha amesema Finland imekuwa, ikisaidia Tanzania katika harakati mbalimbali ikiwemo za kupinga vitendo vya Udhalilishaji kupitia UNFPA.
Hata hivyo ameipongeza Taasisi ya Zanzibar Maisha bora foundation kwa kujikita zaidi katika masuala muhimu ya kijamii kama vile kupinga vitendo vya Udhalilishaji.




