Matukio mbalimbali katika picha ya yakionesha Mhe. Kassim Majaliwa(Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo alipotembelea Kituo cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC) kwa lengo la kuangalia Mfum wa N- CARD unavyofanya kazi.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alikaribishwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa. Aidha ziara hiyo imewashirikisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila na Mkurugenzi Mkuu wa UDRT Bw. Waziri Kindamba.
Katika ziara hii Mhe. Waziri Mkuu ameshuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia uwekezaji wa serikali katika sekta ya TEHAMA.
Kupitia uwekezaji huo ni matarajio ya serikali kuwa na kadi moja itakayomwezesha Mwananchi kunitumia katika mahitaji mbalimbali ikiwemo viwanja vya mipira, kivuko cha Kigamboni, pamoja na stendi ya mabasi ya Magufuli Bus Terminal huku nia ya Serikali ni kuona pia N-Card ikitumika kwenye usafiri wa mabasi yaendayo haraka na maeneo mengine kulingana na mahitaji.