Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) zimesaini mkataba ili kutekeleza Mradi wa Uhifadhi wa Maeneo Oevu na Bioanuwai ya Kidakio cha Katuma, Mpanda
Mradi wa IKI Katuma utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya kiasi cha Euro 4,000,000.00 zitakazotolewa nab Serikali ya Ujerumani.
Lengo la mradi IKI Katuma ni kuzijengea uwezo taasisi mtambuka za Sekta ya Maji katika kuimarisha ushirikiano na kubadilishana maarifa ya usimamizi shirikishi wa rasilimali za maji ili kuhakikisha huduma za mifumo ya ikolojia zinatumika kwa maendeleo endelevu.