Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha,Dokta Mussa Chacha akizungumza kuhusu mradi huo jijini Arusha

Mkurugenzi wa nchi kutoka kampuni ya Korea International Cooperation Agency (KOICA) Manshik Shin akizungumza kwenye ufunguzi huo jijini Arusha .



Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Chuo cha ufundi Arusha (ATC) kwa kushirikiana na kampuni ya Korea International Cooperation Agency (KOICA) wamekabithiana rasmi maabara ya ubunifu ya idara ya uhandisi mitambo ambayo itawasaidia vijana kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo chuoni hapo ,Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha,Dokta Mussa Chacha amesema kuwa ,kitendo cha ufunguzi wa maabara ni kikubwa sana kwani ina vifaa vya kisasa na vya kufundishia wanafunzi pamoja na kubuni michoro mbalimbali kwa kutumia ufundi wa hali ya juu.
Aidha amesema kuwa ,mradi huo una dhamani ya dola 28 ,000 ambapo kati ya hizo chuo kimechangia dola 4,000 .
Amesema kuwa , maabara hiyo ina vifaa vya kisasa ambavyo vinafundisha wanafunzi wetu jinsi ya kubuni michoro mbalimbali kwa njia za kisasa kwa kutumia kompyuta za hali ya juu pamoja na printer ambazo zinachora vitu kwa kisasa zaidi .
Dokta Chacha amesema kuwa uhusiano kati ya chuo cha ufundi Arusha na Korea ulianza siku nyingi na kipindi cha mwanzoni walipata mradi mkubwa ambao kazi kubwa ilikuwa ni kuanzisha mafunzo kwa kozi ya Mekatroniki ambapo hao ni mafundi ambao wanaandaliwa kwenda kufanya kazi kwenye viwanda ambavyo vinatumia teknolojia ya hali ya juu ambapo wanakaa na mitambo inafanya kazi na wao wanaielekeza kitu cha kufanya .
Aidha amesema kuwa, baada ya mradi huo kuendelea na kufanikiwa na kuona wanafunzi wanasoma sana ndipo wakaanza mkakati mwingine na wenzetu wa KOICA kwa kuwaleta watu wanaojitolea wenye uwezo mkubwa sana na umahiri mkubwa na kuja kufundisha walimu na wanafunzi .
Amesema kuwa, mwaka uliopita walipata volunteer mmoja ambaye amekaa nao kwa muda wa miaka miwili sasa ambapo kupitia yeye wakapata mradi mwingine wa kuanzisha maabara ya kisasa kwani ni maabara ya kwanza katika nchi ya Tanzania katika vyuo vya elimu.
“Tunaamini kwa kupitia maabara yetu vijana wetu wataweza kujifunza na kuandaa michoro mbalimbali ya vifaa ambavyo vinatumika na kuvitengeneza hivyo vifaa hivyo tunatarajia mafanikio makubwa kupitia mradi huu.”amesema Chacha .
Aidha amefafanua kuwa, maabara hiyo italeta mafanikio makubwa kwa vijana namna ya kuwafanya vijana kuweza kutengeneza vitu vinavyouzika na vyenye umahiri mkubwa na kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa popote watakapokuwa kwani wanapata umahiri wa kutengeneza michoro mbalimbali na kuiunda na kuweza kuiuza na ni mafanikio makubwa sana katika viwanda vyetu.
Mkurugenzi wa nchi kutoka kampuni ya Korea International Cooperation Agency (KOICA) Manshik Shin amesema kuwa,maabara ya kubuni ya 3D na kuimarisha uwezo wa muundo wa 3D kwa uhandisi wa mitambo ya ubunifu utasaidia sana kuongeza ufanisi kwa wafanyakazi pamoja na wanafunzi katika utendaji kazi wao wa kila siku .
Amesema kuwa,kutendo hicho kinaashiria hatua muhimu mbele katika dhamira ya pamoja ya kuongeza ubora wa elimu ya ufundi nchini Tanzania na kuwezesha kizazi kijacho cha wahandisi, wabuni, na wazalishaji.
“Ulimwengu unabadilika haraka,tunaishi katika wakati ambao teknolojia na uvumbuzi huendesha karibu kila nyanja ya maisha na kazi. Katika enzi hii ya dijiti, muundo wa 3D, modeli, na teknolojia za kuchapa sio zana tu, ni ujuzi muhimu..”amesema .
Shin ameongeza kuwa ,kutoka kwa muundo wa magari na utengenezaji hadi vifaa vya matibabu na suluhisho endelevu za nishati, teknolojia ya 3D iko kwenye moyo wa uhandisi wa kisasa na hii ndio sababu Koica ameshirikiana na ATC kuanzisha maabara ya muundo wa 3D wa kukata.
“Maabara hii ina kompyuta za hali ya juu, wachunguzi wakubwa, printa za 3D, na programu muhimu kama vile AutoCAD na SolidWorks pamoja na vifaa vya kufundishia vilivyosasishwa na vikao vya mafunzo vilivyojitolea kwa wanafunzi na waalimu.”amesema .
Amesema kuwa ,zaidi ya wanafunzi 430, pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi wa kike, sasa wanapata moja kwa moja kwenye kituo hiki. Hii ni karibu zaidi ya vifaa, ni juu ya fursa ambapo Wanafunzi katika uhandisi wa mitambo, mechatronics, na uhandisi wa vifaa sasa wataweza kutumia maarifa yao kwa wakati halisi, kupata uzoefu wa mikono ambao unalingana na mahitaji ya tasnia.
“Maabara hii inafungua uwezekano mpya wa kutoa masomo ya maingiliano, ya kujishughulisha, na ya vitendo ambapo Waalimu sasa wanaweza kufundisha na zana zinazoiga mazingira halisi ya muundo wa ulimwengu, kuwasaidia kujenga uwezo ambao soko la kazi la leo linahitaji.”amesema Shin .
Amefafanua kuwa ,mradi huo unaboresha ustadi wa vitendo katika kubuni na utengenezaji wa 3D, na unawasaidia vijana wa Kitanzania kuwa na ushindani zaidi katika soko la kazi na tayari kwa kazi katika tasnia zinazoendeshwa na uvumbuzi kwa kuongezea, tunakuza ujasiriamali, kuwapa wanafunzi nafasi ya kubuni, mfano, na hatimaye hata kuzindua bidhaa zao na wanaoanza.