Na Oscar Assenga,TANGA
WANANCHI wanaoishi kwenye maeneo yanayostahimili kilimo cha Pamba wametakiwa kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo ambalo ni la kimkakati la kibiashara kutokana na kwamba linaweza kusaidia kupunguza kiasi cha umaskini kwenye ngazi ya kaya,wilaya na Taifa kwa ujumla
Hayo yalisemwa jana na Afisa wa Bodi ya Pamba Tanzania Alphonce Ngawagala wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 12 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Alisema kwamba lengo la wao kushiriki kwenye maonyesho hayo ni kutangaza fursa zinazopatikana kwenye bodi hiyo kwa kuwaelimisha wananchi maeneo gani yanafaa kulima pamba na pembejeo zinapatikana kwa utaratibu upi ambao ni bure.
Alisema kwamba pia baada ya mkulima na kuvuna wanaanzisha soko la mkulima ili aweze kuuza mazao yake kwa wakati ili aongeze kipato chake apate awekeze kwenye mambo mengine ya kimaendeleo.
Aidha alisema kwamba bodi hiyo imepewa dhamana ya kusimamia usindikaji,uzalishaji na kusimamia masoko pamoja na kuelimisha wananchi maeneo yanayotakiwa kulimwa pamba na pembejeo zinapatikana kwa utararibu upi ambao ni bure na baadae ya kulima hizo wao wanasimamia soko ili wakulima wauze.
“Lakini uchakataji wa Pamba inapokwenda kiwandani napo bodi ipo kwa ajili ya kusimamia inasimamia kuhakikisha shughuli zote zinafuata utaratibu, sheria na kanuni zilizowekwa ikiwemo kuangalia ubora na usafi unapatikani”Alisema
Alisema wanafanya hivyo ili kumuwezesha yule mchambuaji baada ya kumaliza taratibu zake aweze kupata kibali kama maborota yake yanapelekwa nje ya nchi apeleke kwa wakati kwa kukamailisha tararibu zote.