Mkuu wa kitengo cha Huduma za Wateja binafsi,Wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMES) ,Joyce Malai akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Mkuu wa Tawi la benki ya Access Arusha ,Edna Kallape akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao katika maonesho hayo jijini Arusha.
……..
Happy Lazaro,Arusha .
BENKI ya ACCESS yenye makao yake makuu jijini Dar es Saalam imeshiriki kikamilifu katika maonesho ya kimataifa ya utalii ya KARIBU-KILIFAIR yanayoendelea jijini Arusha huku wakiwataka wananchi pamoja na wadau wa utalii kufika katika banda lao kujionea huduma na fursa mbalimbali za utalii zinazotolewa .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ,Mkuu wa kitengo cha Huduma za Wateja binafsi,Wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMES) ,Joyce Malai amesema kuwa ,benki hiyo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo mikopo ya magari kwa wadau wa utalii lengo likiwa ni kukuza sekta ya utalii nchini.
Amesema kuwa, kwa Tanzania wana matawi yao katika mkoa wa Arusha,Mwanza ,Dar es Saalam na Dodoma ambapo wapo katika nchi 24 na kati ya hizo nchi 16 ni za Afrika.
Malai amesema kuwa, wanatoa huduma kwa watu wote kwa ujumla ambapo wana kitengo cha huduma binafsi , wafanyabiashara wadogo na wa kati na wakubwa.
Amesema kuwa ,katika banda lao utapata fursa ya kusikia huduma ambazo wanatoa kuanzia huduma ambazo wanazo kwa ajili ya kuongeza faida kwani wapo katika kampeni ya “deposit kwa wateja wote.
Ameongeza kuwa ,benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo mbalimbali kuanzia wafanyakazi wa serikali wateja binafsi,.
“Kwa wateja wetu ambao wangependa kututembelea katika moanyesho haya na kuweza kupata huduma tunazotoa tupo banda la block M.”amesema Malai.
“Huduma zetu kwa Tanzania tupo Arusha, Dodoma ,Dar es Salaam na Mwanza wana matawi sita hadi sasa hivi ,wana satellite ofisi ambazo wanazitumia kwa kwa wafanyakazi wa serikali ambapo wanapatikana kila manispaa Tanzania na wanatumia mawakala pia na matarajio yao ni kuwa wakubwa zaidi na kuweza kuwa katika tano na kumi bora hapo mbeleni .”amesema.
“Kuhusu mikopo wafanyakazi binafasi wanaongea na waajiri lakini kuhusu mtu binafsi wanawahudumia pia ,ambapo kwa upande wa wafanyabiashara ambao ni SMES wanatoa mikopo ya muda mfupi na muda mrefu ambazo zinawasaidia katika biashara zao.”amesema Malai.
Ameongeza kuwa ,Benki ya Access kwa nchi za Afrika wapo katika nchi 16 ambapo kabla ya mwisho wa mwaka wataongeza nchi ya Uganda na wanatoa huduma katika bara lote la East Afrika ,huku kwa nje ya bara la Afrika pia wana shemu ambazo Acces ipo ikiwemo UK,Lebanon,nk na wanatamani kuwapata waafrika na kuwapata katika trade na wamejaribu kutoka nje ya bara la Afrika na kuwa tayari kuwahudumia watanzania na waafrika kwa ujumla nje ya Afrika .
:Utagungua kuwa ukiangalia sana mabenki ya kigeni mengi yanaondoka Afrika na ndio maana Access inaendelea kujikita kuhakikisha inakuwa na matawi kuweza kuisaidia Afrika na nje ya Afrika .”
Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la benki ya Access Arusha ,Edna Kallape amesema kuwa ,mwaka huu wameamua kuja kwenye maonesho hayo ya karibu fair kwa ajili ya kuja kuwaonyesha wanaArusha pamoja na watanzania kwa ujumla bidhaa wanalizonazo kwa ajili ya kuendeleza utalii ambapo wamewiwa kufanya hivyo kwani Guide no moja ni Rais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa hiyo na sisi kama benki tumekuja na bidhaa ambazo zinaenda kuwaongezea dhamani wadau wa utalii.
Amesema kuwa wana bidhaa ambayo ni ya magari ambapo magari hayo wanawapa wanaofanya shughuli za utalii (Tour operators).ambapo wanapewa yakiwa mapya kabisa kutoka kwa massuplying ambapo ndani ya mwezi mmoja mpaka mwezi na nusu wanakuwa wamepata magari yao.
Amesema kuwa ,hii inaendelea kuongeza mnyororo wa dhamani kwenye utalii kwa ajili ya kuwasafirisha watalii kwenda mbugani kwa urahisi zaidi.
“Lakini pia tunawapa mikopo ya project finance wale ambao wanataka kuongeza mnyororo wa dhamani kwani wameona wizara ya utalii imejipanga kwenda kuongeza watalii kuwa milioni 5 na wameona kuna upungufu pia wa vyumba vya malazi hivyo kama Acces Benki Tanzania tumekuja na bidhaa ya kuwaongezea uwezo kwenye kutengeneza hizo camps na lodges na hotel ambazo watalii ndio wanapofikia .”amesema .
“Kwa maana hiyo tunatoa tena na project finance ambao ni mkopo unaowawezesha kujenga lodges ,camps,kuhusani kipindi hiki ambacho tupo mwezi wa sita ambao seccion imeanza hivyo tunawakaribisha sana kwenye banda letu la Access ili waweze kupata huduma hizo .”amesema Kallape.
Ameongeza kuwa ,kwa wananchi wa kawaida kwa wanaArusha wameleta kadi za “Pre -paid “ambapo kadi hizo zinawawezesha wanaArusha kutembea sana na wanakuwa nje ya nchi kutokana na uhalisia wa uchumi wa mkoa wetu ambao unaingiliana na utalii na majirani wa nje ya nchi ambapo kadi hizo zinawasaidia wakisafiri kwenda nje wanaweka pesa na wanapata moja kwa moja kwenye kadi zao .
Amesema kuwa wana card za currency tano kuanzia ya dola,euro ,kadi ya GBP,Zari,na kwa wale wanaobahatika kwenda China wana kadi zao pia na kadi ya currency ya Tanzania ambapo kadi hizo zinaendelea kuwapa dhamani wana utalii wanaposafiri nje ya nchi au wale wazazi wanaposomesha watoto wakiwa nje ya nchi kwa ajili ya kulipia malazi kufanya shopping zao na kadi hizo zinahusika sana kikubwa wazazi wanahusika tu kuweka hela kwenda benki na mtoto kule nje ya nchi anakuwa na nafasi ya kuweza kulipia malazi ,insurance, na zile gharama zote ambazo mtoto anambatana nazo akiwa masomoni nje ya nchi .
“Karibu sana Acces benki kwani ni benki yenu ni benki ya kila mtu kwa sababu wamejipanga kuchukua kila aina ya mteja .”amesema Kallape.