Meneja site Joshua Yohana akionyesha bidhaa mbalilmbali.zinazopatikana kwenye kampuni hiyo jijini Arusha.

Meneja site wa kampuni hiyo Joshua Yohana akitoa maelezo kwa mgeni aliyewatembelea banda lao kujua huduma wanazotoa


………….
Happy Lazaro, Arusha
Kampuni ya Gadgetronix(GX) iliyopo jijini Arusha inayojishughulisha na utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo ya umeme jua imekuja na suluhisho kwa wadau wa utalii wenye Lodges na Camps kwa kuja na Semitrela ya matairi mawili yenye mfumo wa umeme jua unaotembea “Portable solar power system “.
Aidha programu hiyo wamekuja nayo kwenye maonesho ya utalii ya KARIBU-KILIFAIR mwaka huu ambapo kwa mwaka jana walikuja na system yenye tairi moja hivyo kwa mwaka huu wamejipanua zaidi kulingana na mahitaji ya wateja wao.
Aidha kifaa hicho ambacho ni “Portable solar power system “kimetengenezwa kwa kulenga Camps zote zinazohamishika (moving camps).
Aidha system hiyo ni kwa ajili ya Camps ambazo zinahamahama na unapoweka mahema unaweka miundombinu ya maji umeme sasa unapotaka kuhama inakulazimu kuanza kuondoa hivyo vitu hali ambayo ni changamoto kubwa sana kutokana na kutumia gharama kubwa ya kuanza kuhamisha vitu mbalimbali ila uwepo wa system hiyo unarahisha kuhama nayo.kama.ilivyo kwani ni semitrela lenye matairi mawili na bila kuathiri chochote.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo ,Meneja site,Joshua Yohana amesema kuwa ,kampuni hiyo inajihusisha na utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa ajili ya watanzania ambayo inahusisha maswala ya sola.
“kwa mwaka jana tulikuja na kifaa hicho kikiwa na tairi moja na tulifanikiwa kuuzia wateja na mrejesho ulikuwa mzuri sana.”amesema .
Amesema kuwa, kwa upande wa sola wamekuwa wakifanya na wateja hasa upande wa lodges na Camps ambazo zipo kwenye hifadhi mbalimbali Serengeti,Tarangire,Ngorongoro, ambapo wamekuwa wakiwafungia sola kwa ajili ya kupata umeme jua kwenye maeneo yao .
Amesema kuwa, sola hizo zinakuwa na uwezo mbalimbali na hivyo wanafungia wateja wao kulingana na uhitaji wa mteja mwenyewe.
Ameongeza kuwa, endapo mteja atahitaji power system ya sola kwa ajili ya kuhudumia lodge nzima huwa wanawafungia kwa ubora wa hali ya juu na kuweza kuhudumia wageni wao .
“Zaidi sisi tunawafikia mtu mmoja mmoja kuanzia mtu binafsi, ofisi, viwanda,na biashara na kwa wananchi wa kawaida pia wanakuwa suluhisho za changamoto mbalimbali kulingana na uhitaji wa mteja mwenyewe .”amesema .
“Katika maeneo ya vijijini tumeweza kufunga sola nyingi sana na kuwezesha wananchi kutotumia jenereta badala yake wanatumia sola kwa ajili.ya matumizi yao mbalimbali .”amesema Joshua .
Aidha amesema kuwa kampuni hiyo.imekuwa ikifunga sola,geti za umeme,inteneti ,kufunga kamera za ulinzi, kufunga mifumo ya maji moto wa jua,pump za jua ,na pia wanafunga taa za barabarani za sola na umeme ,wanauza friji za umeme na sola na wanatoa huduma ya umeme jua unaotembea na pia wana chumba cha baridi .
Amefafanua kuwa ,wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali na mikoa.yote kutokana na huduma nzuri wanayotoa ambapo wana matawi yao Zanzibar ,Dar es Salaam,na nchini Kenya pia .
Amesema kuwa wamekuwa wakitoa suluhisho la changamoto mbalimbali kwani wanachofanya kwa wateja wao ni kuuza suluhisho la changamoto za wateja wao.
“Tulifikia hatua ya kuja na hiki kifaa ambacho ni trela yenye system zote za umeme wa jua ambacho kitamwezesha kuhama nacho popote pale anapohitaji kwenda bila gharama yoyote na kwa muda muafaka ambapo system ya mwaka huu ina KW 24 na inaweza kubeba WAT 24,000,
hii inakupa umeme kambini na inatumika.maeneo ambayo hakuna umeme kabisa .
Ameongeza kuwa, hiyo system inaendeshwa na umeme jua na ikatokea jua hakuna system hiyo inaingiliana na jenereta.