Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Money, Adolf Kasegenya akibonyeza kitufe kwaajili ya kuzindua Kadi ya Airtel ya Kidijitali ya Global Pay kwa Malipo ya Kimataifa, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam jana Juni 11, 2025 usiku jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Money, Adolf Kasegenya akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua Kadi ya Airtel ya Kidijitali ya Global Pay kwa Malipo ya Kimataifa, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam jana Juni 11, 2025 usiku jijini Dar es Salaam.
Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Airtel Kadi ya Kidijitali ya Global Pay kwa Malipo ya Kimataifa.
* Malipo ya kimataifa bila usumbufu
*Airtel Money yatinga kimataifa
KATIKA hatua kubwa ya kuimarisha matumizi ya teknolojia na ujumuishaji wa kifedha, kampuni ya Airtel Money Tanzania kwa ushirikiano na Mastercard na kampuni ya teknolojia ya Network International, imezindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Global Pay kadi ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kufanya malipo ya kimataifa kwa urahisi, usalama na bila kuwa na akaunti ya benki.
Huduma hiyo mpya, inayopatikana moja kwa moja kupitia MyAirtel App, imebuniwa kusaidia Watanzania kulipia huduma mbalimbali za kimataifa kama vile ada za masomo, bidhaa, usafiri, na burudani kwa kutumia simu ya mkononi, huku wakiweka salio moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money.
Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika jana Juni 11, 2025 katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Money, Adolf Kasegenya, alisema huduma hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali wa dunia.
“Airtel Money Global Pay ni hatua ya mageuzi ya kweli. Inatoa njia salama na ya kisasa ya kufanya malipo ya kimataifa hata kwa wale wasiokuwa na akaunti ya benki,” alisema Kasegenya.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, alisisitiza kuwa huduma hiyo inafungua milango ya dunia kwa mamilioni ya Watanzania.
“Kupitia Global Pay, mteja anahitaji tu kupakua MyAirtel App, kuomba kadi, kuweka salio, na kuanza kutumia huduma kimataifa. Ni rahisi, ni salama, na inapatikana kwa wote,” alisema Rugamba.
“Hii si kadi tu – ni pasipoti ya kidijitali kwa dunia ya fursa,” aliongeza.
Huduma ya Airtel Money Global Pay inaleta mageuzi kwa kutoa suluhisho kwa changamoto zilizowakabili watumiaji wa huduma za mtandaoni kwa muda mrefu ikiwemo ukosefu wa kadi zinazokubalika kimataifa, ukosefu wa uwazi wa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni, na gharama kubwa za miamala. Sasa, kupitia huduma hii.
Watumiaji wanaweza kupata kadi papo hapo bila kwenda benki Kuweka na kutoa salio kwa haraka kupitia Airtel Money Kudhibiti matumizi kwa wakati halisi kupitia App Kufanya malipo popote Mastercard inakubalika kimataifa Ushirikiano wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Ndani.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Telco EEMEA, Kirsten Wottman, alieleza kuwa huduma hiyo ni sehemu ya mkakati wa Mastercard kupanua huduma za kifedha salama kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania.
“Lengo letu ni kuwawezesha Watanzania kuwa sehemu ya uchumi wa dunia kwa njia salama na rahisi, bila kizuizi cha miundombinu ya jadi ya kifedha,” alisem Wottman.
Jinsi ya Kupata Airtel Money Global Pay
*Pakua MyAirtel App kutoka Google Play au App Store
*Ingia kwenye sehemu ya Airtel Money kwa kutumia PIN
*Chagua Global Pay Card
*Kubali vigezo na masharti
*Weka salio kutoka kwenye akaunti yako ya Airtel Money tumia kadi yako kwenye tovuti au majukwaa ya kimataifa
Kwa mara nyingine, Airtel Money imeonesha kuwa inasonga mbele na wakati kwa kuleta huduma zinazoweka nguvu mikononi mwa Mtanzania wa kawaida kuishi, kununua na kulipa kidijitali popote duniani.