Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akiongoza Mkutano wa wadau wa afya kujadili ujenzi wa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na sekta binafsi, limefanya mkutano muhimu wa wadau wa afya kujadili na kukubaliana juu ya ujenzi wa Kliniki ya kwanza ya Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) katika Mkoa wa Shinyanga.
Kliniki hiyo itajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, na itaanza kujengwa kati ya Julai hadi Septemba 2025.

Mkutano huo umefanyika Juni 19,2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ukihusisha viongozi kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), pamoja na Benki ya CRDB, ambayo inafadhili ujenzi huo kwa gharama ya TZS 136,751,920.
KLINIKI MPYA KUWA SULUHISHO ENDELEVU
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa THPS, George Anatory, amesema Kliniki hii itakuwa ya kwanza ya aina yake katika mkoa wa Shinyanga na itatoa huduma maalum kwa watu wanaotumia dawa za kulevya aina ya opiodi (OUDs), pamoja na huduma za kinga na tiba dhidi ya VVU, uchunguzi wa magonjwa sugu na usaidizi wa kitabia.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa THPS, George Anatory.
“Ujenzi wa kliniki hii mpya utakaoanza Mwezi Julai hadi Septemba 2025 ni hatua ya mabadiliko kwa mkoa huu. Itatoa mazingira salama na rafiki kwa watu wanaokabiliwa na matumizi ya dawa za kulevya kupata msaada wa kitabibu, ushauri nasaha, na huduma za marekebisho ya tabia”,amesema.
USHIRIKIANO WA WADAU NA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI
Kwa upande wake , Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Luther Mneney, amesema: “Mpango huu unaonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kukabiliana na changamoto kubwa za kiafya. Tunajenga jamii yenye afya bora inayochangia maendeleo ya taifa.”
Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Luther Mneney.
Mradi huu utatekelezwa kwa msaada wa kiufundi kutoka THPS, usimamizi kutoka Wizara ya Afya, TAMISEMI na DCEA, na ufuatiliaji wa utekelezaji kuhakikisha huduma ni bora na endelevu.
MAONI YA VIONGOZI WA SERIKALI
Mratibu wa Afya ya Akili kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Erasmus Mndeme amesisitiza kuwa kutoa huduma bora za MAT si suala la afya tu bali ni haki ya msingi ya binadamu hivyo Wizara inaunga mkono kikamilifu juhudi hizi.
Kwa upande wake,  Mratibu wa Afya ya Akili TAMISEMI, Bw. Karidushi Charles Kubingwa amesema Kliniki hiyo itapunguza mzigo kwa wananchi wanaolazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma akisisitiza kuwa ni hatua ya kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.
 Dkt. Yudas Ndungile.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, ameongeza kuwa, hiyo itakuwa ni kliniki ya mfano kwa mikoa mingine.
 
“Ujenzi huu inaonesha jinsi  gani taifa linavyoweza kutumia afua za kiafya kukabiliana na changamoto ya dawa za kulevya”,amesema Dkt. Ndungile.
UZITO WA TATIZO NA UMUHIMU WA KLINIKI YA MAT
Kwa mujibu wa Ripoti ya Hali ya Dawa za Kulevya 2023 iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), mnamo mwaka 2023, vituo vyote vya kutolea huduma za MAT nchini vilitoa huduma kwa watu 15,912, huku vitengo vya afya ya akili katika vituo vya kutolea huduma za afya vikiwahudumia takribani watu 903,062 waliokuwa na changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya (SUDs).
Katika Mkoa wa Shinyanga pekee, watu 28,570 walipata huduma kupitia vitengo vya afya ya akili—ambapo asilimia 52.1 (14,885) walikuwa wanawake na asilimia 47.9 (13,700) wanaume.
Kwa sasa, huduma za MAT mkoani Shinyanga hutolewa kupitia vituo vya muda visivyo maalum kwa huduma hizo, hali inayopunguza upatikanaji, faragha, na ubora wa huduma kwa watu wanaotumia dawa za kulevya.
Kukosekana kwa kituo maalum kumesababisha foleni ndefu, ukosefu wa msaada wa kisaikolojia, na changamoto katika uratibu wa huduma hizo.
Kliniki hii ya MAT inatarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma mwanzoni mwa mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya mfumo wa huduma za afya wa Manispaa ya Shinyanga. Wadau wa mkutano wamekamilisha ratiba ya utekelezaji, mikakati ya rasilimali, na mfumo wa uratibu wa huduma.
Kuhusu Huduma za tiba kwa waraibu (MAT)
Huduma za MAT ni huduma za afya zinazolenga watu wanaotumia dawa za kulevya, hasa wanaotegemea dawa za kulevya aina ya opioidi kama heroini.
Huduma hii hutumia mchanganyiko wa dawa maalum, ushauri nasaha na tiba ya kisaikolojia ili kusaidia watu kuacha au kupunguza matumizi ya dawa hatarishi na kuimarisha afya zao.
Kuhusu THPS
Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa nchini Tanzania na kusajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002, lenye dhamira ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa Watanzania wote.
Tangu mwaka 2011, THPS imekuwa ikishirikiana wa Serikali ya Tanzania katika kuimarisha mifumo ya afya na jamii kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yale yamlipuko, magonjwa yasiyoambukiza, afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga, vijana na watoto, pamoja na kuondoa vikwazo vya kimuundo katika upatikanaji wa huduma za afya.
Kupitia ushirikiano wa kimkakati na mbinu zinazotokana na utafiti wa kisayansi, THPS inaendelea kuchangia katika maboresho ya afya endelevu na kushirikiana katika kuandaa na kutathmini afua za afya ya umma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akiongoza Mkutano wa wadau wa afya kujadili ujenzi wa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akiongoza Mkutano wa wadau wa afya kujadili ujenzi wa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akiongoza Mkutano wa wadau wa afya kujadili ujenzi wa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akiongoza Mkutano wa wadau wa afya kujadili ujenzi wa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa THPS, George Anatory akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa afya kujadili ujenzi wa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga

Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Luther Mneney akizungumza kwenye mkutano huo
Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Luther Mneney akizungumza kwenye mkutano huo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akiongoza Mkutano wa wadau wa afya kujadili ujenzi wa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga
Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa kliniki ya  tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga, Mhandisi James Niwagila akionesha ramani ya jengo la MAT
Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa kliniki ya  tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga, Mhandisi James Niwagila akionesha ramani ya jengo la MAT
Mratibu wa Afya ya Akili TAMISEMI, Bw. Karidushi Charles Kubingwa akizungumza kwenye mkutano huo
Mratibu wa Afya ya Akili TAMISEMI, Bw. Karidushi Charles Kubingwa akizungumza kwenye mkutano huo
Mratibu wa Afya ya Akili TAMISEMI, Bw. Karidushi Charles Kubingwa akizungumza kwenye mkutano huo
Mratibu wa Afya ya Akili kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Erasmus Mndeme akizungumza kwenye mkutano huo
Mratibu wa Afya ya Akili kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Erasmus Mndeme akizungumza kwenye mkutano huo
Mratibu wa Afya ya Akili kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Erasmus Mndeme akizungumza kwenye mkutano huo
Wadau wa afya wakitembelea eneo ambalo patajengwa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga
Wadau wa afya wakitembelea eneo ambalo patajengwa kliniki ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT) Mkoani Shinyanga