Sophia Kingimali
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa rai kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kushiriki na kuhasisha wananchi katika mitaa yao kulinda miundombinu ya umeme kwa maslahi ya taifa.
Rai hiyo ameitoa leo Juni 24,2025 jijini Dar es salaam kwenye kikao kazi cha Tanesco na wenyeviti wa Serikali za mitaa halmashauri za manispaa ya ubungo na kinondoni.
Amesema katika mkoa huo kuna miradi mbalimbali mikubwa ya umeme imejengwa hivyo wanapaswa kuwa wazalendo katika kuilinda.
“Umeme ni ajira,umeme ni maisha lakini pia pato la Taifa hivyo tunapaswa kuwa wazalengo katika kuitunza miundombinu yake kwa maslahi binafsi na nchi yetu”, Amesema Chalamila.
Aidha ameongeza kuw6666a wenyeviti wa mitaa wanaongoza jopo kubwa la wananchi katika mitaa yao hivyo dhamana ya ulinzi na amani ipo mikononi mwao.
“Tunapozungumzia amani ya Taifa letu inatokana na utulivu wa taifa letu lakini amani ya pili inatokana na uwepo wa huduma za kijamii ikiwemo u3meme vinapokosekana utulivu hauwezi kuwepo”,Amesema.
qSambamba na hayo Chalamila am2ewataka wenyeviti hao kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wao ili waweze kuyafahamu hali itakayowapelekea hali itakayowapelekea kuzile kuendozwa na Rais Dkt.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya ubungo Albert Msando ameahidi kushirikiana na wenyeviti wa serikalinkutekeleza kwa wakati maagizo ya serikali na chama na kuahidi kushughulikia kwa haraka changamoto na kero za Tanesco pindi zinapojitokeza.
Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umeme nchini TANESCO Lazaro Twange amesema shirika hilo limejipanga kuwafuata wananchi kuwaunganishia umeme kwenye mitaa yao na sio kusubiri wananchi kufuata huduma hiyo kwenye ofisi za shirika.
” Hivi karibuni kulifanyika mkutana wa Nishati nchini Urusi ambapo tumeelekezwa kuunganisha umeme watu million 1.7 kwa mwaka wakati sasa tunaunganisha umeme watu 500000 hadi 600000 kwa mwaka sasa tutafuata watu kwaajili umepin ya kuungan itzawa nakai to chawali txauma wanatufuata ili kufikia malengo,”amesema.
Pia amewasisitiza na kuwataka wenyeviti kuwa mabarozi wa nushati safi ya kupikia katika mitaa yao kwa kuwaelimisha umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia.
“Tunawaomba wenye viti wa serikali nyinyi ndio mabosi katika mitaa yenu mtusaidie kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwani inasaidia kutunza mazingira yetu lakini pia inagharama nafuu”, amesema.
Mbali na utoaji wa elimu hiyo, Twange amemkabidhi Chalamila na viongozi wachache wa mitaa Jiko la Umeme ambalo linatumia umeme kidogo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Jamii.