Na John Bukuku,
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza rasmi kuendesha mitihani ya kitaaluma ya 31 itakayofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti, 2025, jijini Dodoma.
Akizungumza na wanahabari mapema leo Julai, 4, 2025, Kwenye Maonyesho ya 49 Kimataifa ya Biashara Jijini Dar-es-Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Godfred Mbanyi, amesema kuwa kuwa mitihani hiyo itafanyika katika kituo kimoja tu kilichopo Dodoma, na tayari dirisha la usajili limefunguliwa kupitia tovuti ya PSPTB: https://registration.psptb.go.tz.
“Waombaji wote wenye sifa wanaalikwa kujisajili mapema na kuhudhuria madarasa ya maandalizi kama sehemu ya utayari wao kwa mitihani hiyo,” amesema Mbanyi huku akisisitiza kuwa tarehe ya mwisho ya usajili ni 15 Agosti, 2025.
Amesema kuwa makundi ya watu wanaostahili kuomba kufanya mitihani hiyo kuwa Wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu na kati kwa ngazi za Shahada, Stashahada na Astashahada ya Ununuzi na Ugavi waliomaliza kuanzia mwaka 2024 kurudi nyuma ambao hawajawahi kufanya mitihani ya kitaaluma ya PSPTB.
“Pia Wafanyakazi wa sekta binafsi na umma wanaotekeleza majukumu ya ununuzi na ugavi bila kuwa na cheti cha kitaaluma cha CPSP.
Ameongeza kuwa ahitimu wa fani nyingine kwa ngazi za Shahada, Stashahada na Astashahada au wale wenye sifa za kitaaluma kutoka mabaraza au bodi zinazotambulika na PSPTB.
Amefafanua kuwa Wlatahiniwa waliomaliza ngazi mbalimbali za mitihani ya awali ya PSPTB, ikiwemo Basic Stage II, Foundation Stage I & II, na Professional Stages I–IV ndani ya miaka mitano kwa mujibu wa mtaala wa bodi.
Pia Watahiniwa wanaorudia baadhi ya masomo ndani ya miaka mitatu kwa mujibu wa mtaala mpya wa kitaaluma.
Mbanyi aliongeza kuwa watahiniwa wanaorudia mitihani zaidi ya ngazi moja wanaruhusiwa kuunganisha ngazi mbili zinazofuatana (Two Consecutive Blocs), kwa idadi ya masomo isiyopungua mawili na isiyozidi sita, lakini kwa kuzingatia ratiba rasmi ya mitihani hiyo ya 31.
Kuhusu ada za mitihani, PSPTB imeeleza kuwa gharama hizo zimewekwa wazi kwenye tovuti ya Bodi, na imewasihi waombaji kutembelea tovuti hiyo kwa maelezo zaidi. Vilevile, Mbanyi alieleza kuwa mitihani mingine ya kawaida inayofanyika mwezi Novemba na Mei itaendelea kama kawaida.
Ameongeza kuwa Kwa maelezo au ufafanuzi zaidi, waombaji wanashauriwa kuwasiliana na Bodi kupitia
Simu: 0738 441 972
Barua pepe: examinations@psptb.go.tz