Mwenyekiti wa Kikao cha kujadili Awamu ya Pili ya Utekelezaji Mradi Kabambe wa Kuboresha Takwimu nchini (TSMPT II) ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiongoza kikao hicho jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza Dkt. Juma Malik Akil na kushoto ni Mtakwimu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Amina S. Msengwa.
Na Mwandishi Wetu
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekutana kujadili utekelezaji pamoja na kupitisha Mpango Kazi wa Awamu ya Pili ya Mradi Kabambe wa Kuboresha Takwimu nchini (Tanzania Statistical Master Plan-TSMPT II).
Kikao hicho cha kujadili mradi wa TSMPT II kimefanyika jijini Dodoma jana chini ya mwenyekiti wake ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt Natu El-maamry Mwamba. Mradi huo wa TSMPT II unatekelezwa katika kipindi cha mwaka 2022/23 hadi 2026/27.
Awamu ya kwanza ya utekelezaji Mradi Kabambe wa Kuboresha Takwimu nchini (TSMPT I) ulifanyika katika kipindi cha mwaka 2011/12 hadi 2017/18.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mbali na mambo mengine ina jukumu la kutoa takwimu rasmi zilizo bora na huduma zinazokidhi mahitaji ya wadau wa kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kupanga mipango na kufanya maamuzi yenye uthibitisho.
Mwenyekiti wa Kikao cha kujadili Awamu ya Pili ya Utekelezaji Mradi Kabambe wa Kuboresha Takwimu nchini (TSMPT II) ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiongoza kikao hicho jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza Dkt. Juma Malik Akil na kushoto ni Mtakwimu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Amina S. Msengwa.
Washiriki wa Kikao cha kujadili Awamu ya Pili ya Utekelezaji pamoja na kupitisha mpango kazi wa awamu ya pili ya Mradi Kabambe wa Kuboresha Takwimu nchini (TSMPT II) wakiwa katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 16 Julai 2025.
Mwenyekiti wa Kikao cha kujadili Awamu ya Pili ya Utekelezaji pamoja na kupitisha mpango kazi wa Mradi Kabambe wa Kuboresha Takwimu nchini (TSMPT II) ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na bàadhi ya washiriki mara baada ya kikao kilichofanyika jijini Dodoma.