MKUU wa Mkoa wa Kigoma, IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 19,2025 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
MKUU wa Mkoa wa Kigoma, IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 19,2025 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro,(hayupo pichani) wakati kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
Na Alex Sonna, Dodoma
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Kigoma umepokea jumla ya shilingi trilioni 11.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 731.5 zimetumika kwenye ujenzi wa barabara.
Hayo yamesemwa leo, Julai 19, 2025, jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
Balozi Sirro amesema kuwa awali barabara za kuelekea Kigoma zilikuwa na changamoto kubwa, zikiwa ni za vumbi wakati wa kiangazi na tope kipindi cha masika. Hata hivyo, kwa sasa hali imebadilika kwa kiasi kikubwa.
“Barabara kuu zinazounganisha Kigoma na mikoa ya Tabora na Shinyanga zimejengwa kwa kiwango cha lami na zinatumika kikamilifu. Zingine zipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji,” amesema Balozi Sirro.
Katika sekta ya kilimo, Balozi Sirro amesema kuwa uzalishaji wa zao la chikichi umeongezeka kutoka tani 25,000 mwaka 2020/2021 hadi tani 35,000 mwaka 2024/2025 — sawa na ongezeko la asilimia 40.
“Pia, uzalishaji wa mbegu bora za chikichi aina ya TENERA umeongezeka kutoka mbegu milioni 1.6 hadi milioni 2.9 katika kipindi hicho, sawa na ongezeko la asilimia 85.4,” amesema.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imenunua pikipiki 153, vipima udongo 5, na magari 2 kwa ajili ya maafisa ugani na wakaguzi wa kilimo, ikiwa ni jitihada za kuongeza ufanisi wa huduma kwa wakulima. Aidha, maafisa ugani wapya 93 wameajiriwa mkoani Kigoma, huku wengine saba wakipangwa kupitia programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT).
Kupitia mfumo wa ruzuku ya pembejeo, matumizi ya mbolea mkoani humo yameongezeka kutoka tani 21,780 mwaka 2020/2021 hadi tani 40,296 mwaka 2024/2025, ongezeko la asilimia 85. Hatua hii imesaidia kuongeza tija kwa wakulima wa mazao mbalimbali.
Balozi Sirro amesema idadi ya vyama vya ushirika imeongezeka kutoka kimoja mwaka 2020/2021 hadi vinane mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 700. “Hii imeongeza ushirikishwaji wa wakulima kwenye masuala ya masoko, mikopo na usimamizi wa rasilimali,” amesema.
Katika kuboresha mazingira ya kazi kwa wataalamu wa sekta ya kilimo, serikali imefanikiwa kujenga nyumba nne (4) za watumishi kwenye maeneo ya vijijini, ili kuongeza uwepo wa wataalamu na kurahisisha huduma kwa wakulima.
Aidha amesema kuwa Mkoa wa Kigoma umeendelea kunufaika na uwekezaji wa Serikali katika kukuza utalii, ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vya kitalii kama vile Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Hifadhi ya Taifa ya Mahale, Ziwa Tanganyika pamoja na vivutio vya kihistoria na kiutamaduni kama Kituo cha kumbukumbu ya Dk. Livingstonekilichopo Ujiji.
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita Watalii wa ndani wameongezeka kutoka 630mwaka 2020 hadi 11,769mwaka 2025,Pia, Watalii wa nje wameongezeka kutoka 345mwaka 2020 hadi 655kufikia mwaka 2025.
Aidha Sekta ya madini ina nafasi ya kipekee katika kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni na ukuaji wa uchumi kwa ujumla, Mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa sekta hii ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa dhahabu kutoka gramu Elfu 12.5 mwaka 2020 hadi gramu Elfu 15.2 mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 22
“Kuongezeka kwa fedha za kigeni zilizotokana na uuzaji wa Dola za Marekani Elfu115.4 mwaka 2025 sawa na madini kutoka Dola za Marekani Elfu 22.6 mwaka 2020 hadi ongezeko la asilimia 411”
“Kuongezeka kwa masoko ya madini kutoka SokoMoja (01)ni Soko la zamani la Madini Kakonko na Soko jipya la Madinimwaka 2020 hadi masoko Mawili (02) mwaka 2025 ambayo la Kigoma; na Kuongezeka kwa utoaji wa leseni za uchimbaji kutoka leseni 354 mwaka 2020 hadi leseni 799 mwaka 2025″Ameongeza