Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB, Wakili Patrick Kipangula akimkabidhi Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) Mkurugenzi Mtendaji wa Michuzi Media Group Muhidin Issa Michuzi kwa niaba ya Waandishi wengine wanaoendelea kupokea vitambulisho vyao baada ya kukidhi vigezo vya kisheria.
Akizungumza mara baada ya kumkabidhi kitambulisho hicho Wakili Kipangula amempongeza Michuzi na Waandishi wengine waliokwishakupokea vitambulisho vyao baada ya kukidhi vigezo huku akitoa wito kwa Waandishi ambao bado hawajapata vitambulisho vyao kuingia katika mfumo kuhakiki viambatisho walivyoweka kama vipo na vinafunguka kabla ya kupiga simu Bodi kuulizia hali ya maombi yao.
Amesema maombi mengi yana mapungufu ya viambatisho hivyo kutosoma, kuonekana kiambatisho kimoja, kujirudia kwa kiambatisho kimoja, kuweka vyeti visivyotambulika kisheria na wengine barua za utambulisho kutoambatishwa