Timu ya Taifa ya Wanawake ya Nigeria inatarajia kushuka dimbani usiku wa leo dhidi ya Timu ya Taifa ya Morocco kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake WAFCON katika dimba la Olympic Stadium Rabat Nchini Morocco.
Morocco ilifanikiwa kufika kufika hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju 4-2 ya penati dhidi ya Ghana kufuatia sare ya b1-1 huku Nigeria ikitinga fainali baada ya kuwaondosha mabingwa watetezi wa taji hilo Afrika Kusini kwa kuifunga magoli 2-1.
Mabingwa mara 9 wa michuano hiyo Nigeria inahitaji kulipa kisasi kwa Morocco na kutwaa taji hilo kufuatia kichapo walichowahi kukipata cha mikwaju ya penati mwaka 2022 na kuondoshwa na Morocco katikaa mchezo wa nusu fainali ya mashindano hayo.
Je Morocco watafanikiwa kubeba ubingwa wa kwanza wa mashindano hayo au Nigeria watafanikiwa kuongeza kombe la 10 la WAFCON katika kabati lao la makombe.