AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa Fadlu yupo likizo ila anafanya kazi kwa moyo mkubwa akiwa Tanzania.
“Katika vitu ambavyo tunapaswa kujivunia kwa hali na mali Wanasimba ni uwepo wa Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Yupo likizo lakini alitoka Afrika Kusini na kuelekea Dubai kuongea na Mo.
“Kwa sasa Fadlu yupo Tanzania akifuatilia hatua kwa hatua wachezaji atakaowasajili na kufanya mipango ya msimu ujao. Anafanya kazi kwa moyo mkubwa mno katika kutimiza majukumu yake. Wanasimba tunapaswa kujivunia kuwa na kocha huyu,”.
Simba SC msimu wa 2024/25 ilikuwa chini ya Fadlu ambaye dakika 180 mbele ya Yanga SC kwenye mechi za ligi zote alipotea mzunguko wa kwanza na ule wa pili.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC na mzunguko wa pili, Yanga SC 2-0 Simba SC. NI mechi mbili alipoteza baada ya kucheza mechi 30 msimu uliopita wakigotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.