MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC Jean Ahoua huenda akaondoka ndani ya Bongo kwenda kupata changamoto mpya.
Inaelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC raia wa Ivory Coast, Ahoua yupo kwenye rada za Klabu ya JS Kabylie ya nchini Algeria kwa ajili ya msimu ujao wa 2025/26.
Habari zinaeleza kuwa kuna mazungumzo ambayo yanaendelea kati ya Simba SC na timu ambayo inamuhitaji mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wake wa kulia katika kufunga.
Ahoua ni namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi alifunga jumla ya magoli 19 na kutoa pasi 9 za magoli akiwa na uzi wa Simba SC msimu wa 2024/25.
Ikiwa dili litajibu Ahoua anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili kutoka katika Ligi Kuu Tanzania Bara kujiunga na JS Kabylie, mwingine ni kiungo mchezeshaji, Arthur Bada aliyejiunga na kikosi hicho akitokea Singida Black Star.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC hivi karibuni aliweka wazi kuwa kwa mchezaji ambaye watakuwa hawana mpango naye watamuuza ila wakiwa na mpango naye hawatamuuza.