CHE Malone ndo basi tena ndani ya kikosi cha Simba SC baada ya kupata changamoto mpya nje ya Tanzania hivyo msimu wa 2025/26 hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Che Malone anatajwa kupata timu nchini Algeria kwa ajili ya changamoto mpya na tayari Simba SC wamempa Thank You beki huyo aliyekuwa chaguo la kwanza kikosi cha Simba SC.
Mrithi wa Che Malone ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Simba SC raia wa Afrika Kusini ambaye aliwahi kucheza Mamelod Sundowns anaitwa Rushine De Reuck.
Julai 30 2025, Che Malone amekutana na Thank You hivyo hatakuwa ndani ya Simba SC kwa msimu ujao kwenye mechi za ushindani.
Beki mpya ambaye ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Simba SC yupo kwenye msafara wa Simba SC uliokwenda Misri kwa maandalizi ya msimu ujao wa 2025/26.