Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Morice Abraham amejiunga rasmi na wekundu wa msimbazi kama mchezaji wao kuelekea msimu ujao wa mashindano akitokea Spartak Subotica ya Serbia kwa mkataba wa miaka miwili.
Morice ambaye amefanya mazoezi na timu ya Simba mwishoni mwa msimu uliopita ni chaguo la kocha Fadlu Davids baada ya kuridhishwa na kiwango chake.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amekulia katika Kituo cha kukuzia vipaji cha Alliance Academy cha jijini Mwanza anakumbukwa kuwa na nahodha wa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kilichoshiriki AFCON mwaka 2019 ambayo Tanzania alikuwa mwenyeji.