AFISA Habari wa Yanga SC Ally kamwe, hatimaye ameaga rasmi maisha ya upweke baada ya kufunga ndoa leo jijini Arusha, katika hafla iliyohudhuriwa na ndugu, marafiki na wadau mbalimbali wa tasnia ya burudani.
Sherehe hiyo ya kipekee ilifanyika katika mazingira ya kuvutia, huku wageni waalikwa wakijawa na furaha na bashasha tele. Alikamwe alionekana mwenye furaha isiyo kifani akiwa na mwenzi wake mpya wa maisha, katika tukio lililosheheni mapenzi, shukrani na baraka tele.