Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Le Havre AC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa (Ligue 1).
Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ amemaliza mkataba na waliokuwa waajiri wake timu ya PAOK Thessaloniki kutoka Ugiriki aliyokuwa aliokuwa akiwatumikia kwa misimu miwili iliyopita.
L’Équipe imeripoti kuwa Samatta tayari amewasili nchini Ufaransa kukamilisha dili hilo la kujiunga na klabu hiyo ya Normandy.
Baada ya kuweka historia nyingi sasa Captain Diego anaenda kuweka Rekodi nyingine mpya ya kuwa mchezaji wa Kwanza raia wa Tanzania kucheza Ligue 1, ambayo Mabingwa watetezi ni klabu ya Paris Saint Germain inayoelezwa kuwa ndio Klabu bora kwa sasa Duniani.