DAR ES SALAAM: Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Hemedi Selemani, amesema kuwa ana imani kubwa na kikosi chake kuelekea mchezo unaofuata wa Agosti 6,2025 dhidi ya Mauritania akisisitiza kuwa lengo kuu ni kupata ushindi bila kujali idadi ya mabao.
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha Hemedi amesema kuwa ushindi ndio jambo la msingi zaidi katika mashindano, akibainisha kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri na wana morali ya hali ya juu.
“Naamini sana katika kupata ushindi haijalishi tutafunga magoli mangapi cha msingi ni kupata ushindi,” amesema kocha Hemedi.
Akiwashukuru Watanzania kwa hamasa waliyoionesha katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Burkina Faso, Hemedi ametoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuendelea kuwaunga mkono katika mchezo dhidi ya Mauritania.
The post ‘Tunahitaji nguvu ya Watanzania kesho’ first appeared on SpotiLEO.