KLABU ya Azam FC ya Tanzania imepangwa kucheza na El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini kwenye hatua za awali michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
KMKM ikipangwa kucheza dhidi ya AS Port ya Djibouti. Azam FC msimu wa 2024/25 ilikuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu itakuwa katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) ambapo Tanzania inawakilishwa na klabu tatu jumla. Klabu mbili kutoka Tanzania bara na moja kutoka Zanzibar.
Singida Black Stars ya Tanzania kwenye anga la kimatafa itaanzia ugenini ambapo kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Ni Rayon Sports ya Rwanda kwenye anga la kimataifa imepangwa kucheza na Singida Black Stars ambapo ni Singida Black Stars watakuwa ugenini.
Agosti 9 2025 droo imechezwa katika studio za Azam TV, Dar ikiwa ni hatua za awali kwenye anga la kimataifa msimu mpya wa 2025/26.