DAR ES SALAAM, MABINGWA wa soka la Tanzania Yanga SC wamepangwa na klabu ya Wiliette Banguela ya Angola Katika raundi ya kwanza ya hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika inayotarajiwa kuburudisha mashabiki wa soka kote barani Afrika baadaye mwezi Septemba.
Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara wanaingia katika michuano hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kuishia hatua ya makundi msimu uliopita huku wakiwa na lengo la kufikia hatua ya makundi ya michuano hiyo msimu huu
Mshindi wa mtanange huo atakutana na mshindi wa mtanange kati ya Elgeco Plus ya Madagascar na Silver Strikers ya malawi
Michezo ya raundi ya kwanza ya hatua ya awali inatarajiwa kupigwa kati ya Septemba 19-21 na marudiano kati ya tarehe 26-28 na michezo ya raundi ya pili ya hatua hiyo itapigwa kati ya Oktoba 17-19 na marudiano wiki moja baadaye
The post Yanga yakabidhiwa Waangola CAFCL first appeared on SpotiLEO.