Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amethibitisha ujio wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Sadio Kanoute ambaye anakuja kujiunga na Azam FC.
Kiungo huyo raia wa Mali atawasili kesho nchini kwa ajili tataratibu za mwisho za kujiunga na kikosi hicho cha Azam FC ambacho kwa sasa kipo chini ya kocha Florent Ibenge.