CHAN 2024 | KWENYE mechi tatu [3] zilizopita za Taifa Stars kwenye michuano ya CHAN 2024 ukiachilia mbali kushinda michezo hiyo na kukusanya alama tisa [9], Stars imetoa wachezaji bora wa mechi kwe kila mchezo!
Mchezo wa ufunguzi [Tanzania 2-0 Burkina Faso] Feisal Salum Abdallah ‘Feitoto’ alitangazwa mchezaji bora wa mechi ‘Man of the Match’.
Mchezo wa pili [Mauritania 0-1 Tanzania] Mudathir Yahya Abbas alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi ‘Man of the Match’.
Na mchezo wa tatu [Tanzania 2-1 Madagascar] Clement Frances Mzize akatangazwa mchezaji bora wa mechi ‘Man of the Match’.