MIAMI: MWANAMUZIKI maarufu wa muziki wa Afrobeats David Adeleke, anayejulikana kama Davido, na mpenzi wake wa muda mrefu Chioma Rowland wamefunga ndoa na sherehe kubwa ya harusi yao imefanyika Miami, Florida, nchini Marekani.
Hafla hiyo ya kupendeza iliyofanyika jana Agosti 11, 2025 ilihitimishwa naa hadithi ya mapenzi ambayo imedumu kwa muongo mmoja, shereha hiyo ilivutia mamilioni ya watu ulimwenguni kote.
Katika harusi hiyo wazazi wa Chioma hawakufika kwa kinachodaiwa ni kunyimwa kwa viza za kuingilia nchini humo.
Awali wawili hao walifunga ndoa ya kimila Machi 2023 na sherehe ya kitamaduni ilifanyika katika jiji la Lagos nchini Nigeria mnamo Juni 2024.
Harusi waliyofunga nchgini Marekani ilijumuisha familia ya msanii huyo, marafiki, wasomi wa kisiasa, wafanyabiashara wakubwa ulimwenguni, na wasanii wenye majina kutoka maeneo mbalimbali.
Miongoni mwa matajiri wakubwa waliohudhuria harusi hiyo ni Aliko Dangote, ambaye ni tajiri zaidi barani Afrika na Godfather Davido, ambaye inasemekana alisafiri kwa ndege ndani ya saa 72 tu baada ya kuhudhuria harusi nyingine maarufu nchini Iceland.
Wengine waliohudhuria harusi hiyo ni Ademola Adeleke, Gavana wa Jimbo la Osun na mjomba wa Davido. Wanamuziki waliohudhuria ni pamoja na Adekunle Gold, Teni, D’banj, na mkongwe wa injili wa Marekani Kirk Franklin.
Sherehe hiyo iligharimu dola milioni 3.7. Katika hotuba yake, Davido ambaye alizaliwa nchini Marekani na sasa anatamba na wimbo wa ‘Assuarance’, ‘Unrechable’ na ‘Fall’, alimpongeza mkewe Chioma kwa maneno haya: “Wewe ni mpenzi wangu, amani yangu, nyumba yangu. Ulikuja katika maisha yangu kimya kimya na ukawa sehemu enye sauti kubwa na nzuri zaidi. Uliniona mimi halisi, mimi ambaye ulimwengu hauoni, na bado ulinichagua.”
Maneno ya bwana harusi yaligusa wageni na mashabiki ulimwenguni kote, ambao wengi wao wamekumbuka wanandoa hao walivyofiwa na mtoto wao wa kwanza, Ifeanyi, mnamo 2022.
Katika ishara ya kujitolea kwa milele, Davido alionyesha tattoo mpya ya ‘Chioma’ iliyokuwa na wino kwenye sehemu ya chini ya tumbo lake wakati wa kupiga picha zao za kabla ya harusi. Akiongeza urembo huo, Davido alimshangaza Chioma kwa saa ya mkononi ya Richard Mille yenye thamani ya dola 300,000, zawadi ya kifahari.
Wanandoa hao maarufu sasa ni wazazi wa watoto wawili, mapacha waliozaliwa Oktoba 2023.
The post Davido, Chioma washerehekea harusi Marekani first appeared on SpotiLEO.