NEW YORK: Mwanamuziki Jessie J amekiri kuhofia kuugua kwa mara nyingine saratani ya matiti.Nyota huyo wa pop mwenye umri wa miaka 37 alifanyiwa upasuaji wa saratani ya matiti katika hatua ya awali mwezi Juni na madaktari walimwambia mwimbaji huyo kuwa wameondoa seli zote zisizo za kawaida, lakini Jessie atahitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara katika siku zijazo kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa huo kurudi.
Mwimbaji huyo ambaye ameratibiwa kufanyiwa upasuaji mwingine ili kurekebisha vipandikizi vyake baadae mwaka huu aliliambia gazeti la The Sunday Times: “Nimepata upasuaji mwingine kuboresha ulinganifu wa upandikizaji kwenye titi langu lingine na ninahitaji kupona, kwa hivyo ni lazima nichunguze mara kwa mara,” amesema.
Jessie aliendelea kufichua kwamba anaona suala la afya yake kama onyo la kupunguza kasi, na kuongeza: “Usiku uliopita, Mama alikuwa akinisugua matiti yangu, kwa sababu siwezi kugusa makovu yangu mwenyewe nina hofu kwani nilianza kulia: ‘Siwezi kuamini kuwa hii imetokea.’
Licha ya yote hayo Jessie amedai ataendelea kuachia wimbo mpya baada ya kupona upasuaji wake.
Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, alieleza: “Nina wiki 7 baada ya upasuaji wa saratani ya matiti. Bado niko katika hali ya kupona na mwili wangu bado unapata nguvu.
“Lakini Napenda muziki na Ninapenda maisha yangu na nataka Kuishi. “Badala ya kusimama na kutoweka na kungoja wakati uwe kamili wa kuachia muziki tena. Ninachagua kuendelea.
“Maisha yamepangwa na yana hali ya juu na ya chini na lazima tuendelee kuishi katika yote, bora tuwezavyo.
“Kwa hivyo niko hapa. Kuishi…” Chapisho la Jessie liliambatana na video fupi.
The post Jessie J ahofia kuugua tena saratani ya matiti first appeared on SpotiLEO.