WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC wameanza kazi kupima kikosi chao wa kupata ushindi kwenye mchezo wa kirafiki.
Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kambi yao ni nchini Misri kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26.
Agosti 11 2025 walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kujipima nguvu na mwisho walipata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo.
Wafungaji kwenye mchezo huo ni wapya ikiwa ni Mohamed Bajaber aliyefunga bao moja katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia uliochezwa Uwanja wa Suez Canal Authority.
Bao jingine ni mali ya mshambuliaji mpya Jonathan Sowah ambaye huyu yupo Simba SC kwa makubaliano maalumu akitokea Singida Black Stars.