LIVERPOOL: MTENDAJI mkuu wa Ligi Kuu ya England Richard Masters ametetea mchakato wa kisheria wa ligi hiyo kufuatia kukosolewa kwa kasi ya uendeshaji wa kesi ya kinidhamu ya Manchester City iliyohusisha mashtaka 115 ya madai ya uvunjaji wa sheria za kifedha.
Akizungumza na Sky Sports kwenye hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa Premier League iliyofanyika jijini Liverpool Masters amesema mara tu mashtaka yanapopekekwa na uongozi wa juu wa Ligi hiyo, jambo hilo hukabidhiwa kwa jopo ambalo hufanya kazi kwa uhuru mkubwa.
“Ni kama mahakama huru tu kimsingi. Likishafika kwao wao husimamia mchakato na muda wake. Wanasikiliza kesi hiyo na watakuwa na maamuzi ya mwisho hatuna ushawishi wowote kwenye uendeshaji au muda watakaotumia.” – alisema Masters
Masters alikataa kuzungumzia ni lini hasa anahisi jopo hilo litafikia uamuzi lakini alikiri kuwa anakerwa na michakato mirefu ya kisheria juu ya swala hilo ambalo limekuwa vinywani mwa wadau wa soka kwa muda mrefu.
“Wasiwasi wangu hauna maana kwakweli, lazima nisubiri tu. Michakato ya kisheria mara chache huchukua muda kidogo kuliko vile ulivyotarajia. Lakini lazima tuwe na subira,” alisema.
The post Kesi za Man City zamuibua CEO wa Ligi kuu first appeared on SpotiLEO.