MUMBAI: MUIGIZAJI nguli kutoka India Amitabh Bachchan amempongeza mwanaye Abhishek Bachchan aliyeshinda tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume iliyotolewa katika Tamasha la Filamu la India Usiku wa Tuzo za Melbourne 2025.
Amita kwa sasa anajiita baba mwenye furaha zaidia duniani baada ya mwanae huyo kushinda tuzo hiyo kupitia filamu ya ‘I Want to Talk’.
Licha ya kuandika hayo akimpongeza motto wake huyo pia ameweka picha wakiwa wawili inayowaonesha wakiwa katika jalada la jarida.
Katika blogu yake, Amitabh alimwita Abhishek “fahari na heshima ya familia”. Akijiita “baba mwenye kiburi sana”, Amitabh alisema;”bei ya ushindi ni kubwa, lakini pia ni thawabu”.
“Mimi ni Baba mwenye furaha zaidi katika Ulimwengu mzima…Abhishek, wewe ni fahari na heshima ya familia.” Aliandika Amita katika blogu yake.
Aliongeza, “Unapeperusha bendera ambayo Dada ji alianzisha, na umeibeba kwa ushujaa na bidii, uthabiti, kutokubali kamwe kushindwa; kadiri unavyonishusha chini, nitasimama tena na bidii yangu na nitasimama juu zaidi.
“Ilichukua muda, lakini haukukata tamaa. Umeonesha ulimwengu kwa sifa yako mwenyewe. Umetangazwa kuwa msanii wa kwanza kwangu kama baba wa kwanza mwenye furaha duniani.” Alimaliza Amita.
The post Mtoto wa Amitabh Bachchan aibuka muigizaji bora India first appeared on SpotiLEO.