BIRMINGHAM: Newcastle United sasa hawajashinda mechi 6 walizocheza bila mshambuliaji Alexander Isak wakishindwa kufunga bao katika mechi nne kati ya hizo. Katika mchezo wa leo dhidi ya Aston Villa, walitawala kwa kiasi kikubwa lakini hawakufunga bao dhidi ya timu yenye wachezaji pungufu baada ya kadi nyekundu ya beki wa kati wa Villa Ezri Konsa.
Mchezo unaofuata Newcastle itacheza dhidi Liverpool nyumbani kwao St James’s Park Agosti 25, Liverpool ambao dau lao nono la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden hivi karibuni lilikataliwa, Newcastle wakitaka pesa zaidi.
“Nadhani kila mara ni ngumu kucheza dhidi ya Liverpool, kuna historia ya mechi, imekuwa mchezo wa kushangaza katika miaka ya karibuni kwenye Premier League, kwa hivyo tuna subiri kwa hamu. Tunawaheshimu tunajua walivyo wazuri, tuko tayari kwa hilo.” amesema kocha wa Newcastle Eddie Howe
Isak anayefanya mazoezi kando na wachezaji wengine na inasemekana amekataa kuichezea tena klabu hiyo tena. Hatua ambayo imetajwa na wadau wa soka kuwa ni kukosa weledi.
Pengo la Isak katika mchezo huo lilikuwa wazi kiasi cha aliyepewa nafasi ya kuliziba Anthony Gordon alipwaya na kukiri ugumu wa majukumu hayo huku akiahidi kubadilika na kuwa mshambuliaji wa kati kama kocha wake atamtaka.
The post Mzimu wa Isak waanza kazi Newcastle first appeared on SpotiLEO.