MECHI ya Simba na Yanga inatarajiwa kuchezwa mapema ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayowakutanisha Yanga SC na Simba SC, Septemba 16, 2025 jijini Dar.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa kwa mwaka huu, Ngao ya Jamii itachezwa kwa mchezo mmoja pekee kufuatia mabadiliko ya kanuni yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji. Awali, mashindano haya yalikuwa yakihusisha nusu fainali mbili na kisha fainali.
Mabadiliko hayo yamesababishwa na msongamano wa ratiba, ikiwemo Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za CHAN zitakazomalizika Agosti 30, pamoja na mechi mbili za mchujo za Kombe la Dunia zinazokabili Taifa Stars mapema Septemba. Mara baada ya Ngao ya Jamii, vilabu vya Tanzania vitakuwa vitani tena kwa michezo ya raundi ya awali ya mashindano ya CAF.
Ipo wazi kwamba msimu wa 2024/25 Ngao ya Jamii ni Yanga SC ilitwaa ambapo ilichezwa kwa mfumo wa kuanzia hatua ya nusu fainali.
Simba SC ilikuwa mshindi wa pili baada ya kucheza na Coastal Union ya Tanga huku Yanga SC ikitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi mbele ya Azam FC.