MASTAA wa kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu,Romain Folz Agosti 19 2025 walikuwa kwenye mazoezi maalumu katika fukwe za Coco Beach Dar kwa lengo la kusaka pumzi na kuwa imara zaidi.
Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
Msimu wa 2024/25 walikuwa chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ambaye alipewa Thank You na mikoba yake ipo mikononi mwa Folz.
Kwenye program ya ufukweni wachezaji walikuwa kwenye kazi kubwa chini ya kocha wa viungo Chyna Mok ambaye aliweka wazi kuwa ni mpango maalumu kuhakikisha kuwa wachezaji wanakuwa fiti asilimia kubwa.
“Malengo yetu ni kuona kwamba wachezaji wanakuwa fiti asilimia kubwa na kila kitu kinakwenda vizuri.Tunahitaji kuwa imara hasa ukizingatia kwamba Yanga SC ni timu kubwa na wachezaji wanatambua hilo,”.
Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye program hiyo ni Fardi Mussa, Bakari Nondo,Pacome, Kibwana Shomari.