DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva Yasrin Yasin ‘Yammi’ ameachia rasmi EP yake mpya iitwayo After All, leo Agosti 22, akipata sapoti kubwa kutoka kwa aliyewahi kuwa meneja wake na msanii maarufu, Faustina Mfinanga ‘Nandy’.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy alishea taarifa za kuachia kwa EP hiyo, huku akimpongeza Yammi kwa hatua hiyo muhimu katika muziki wake.
Ujumbe huo umeibua hisia chanya kutoka kwa mashabiki ambao wametafsiri kitendo hicho kama ishara ya maridhiano na upendo.
Kabla ya hapo, Yammi alikuwa chini ya usimamizi wa Nandy kupitia lebo ya The African Princess, lakini mahusiano yao ya kikazi yalikoma kwa hali iliyoacha maswali mengi kwa mashabiki.
Hata hivyo, sapoti hii mpya inaonesha kuwa wawili hao wameamua kusonga mbele na kuweka tofauti zao pembeni.
Wengi wamepongeza hatua hiyo ya Nandy kama mfano bora wa kuonesha ukomavu na mshikamano ndani ya tasnia ya muziki, huku wakimtakia Yammi mafanikio zaidi kupitia kazi yake
The post Nandy ampongeza Yammi kwa EP mpya “After All” first appeared on SpotiLEO.