Ripoti kutoka nchini Kenya zimesema kuwa Kenya Police FC wamealikwa kumenyana na wababe wa Tanzania, Simba SC katika mchezo wa kirafiki siku ya Simba Day, utakaofanyika Septemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kenya Police FC ni mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya kwa msimu wa 2024/25, ndiyo timu aliyotoka nyota mpya wa Simba Mohammed Bajaber.
Klabu hiyo bado haijathibitisha kushiriki, lakini tayari watakuwa nchini Tanzania kwa ajili ya michuano ya CECAFA Kagame Cup 2025, itakayoanza Septemba 2 hadi 15 jijini Dar.