Meneja Habari na mawasiliano Klabu ya Yanga ametangaza kauli mbiu mpya kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2025/26 ikiwa ni siku chache kabla ya kuazimisha siku ya mwananchi septemba 12 mwaka huu.
“Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa na Slogan za kupeana matumaini, tumekubaliana huu ni msimu wa vitendo na tumegundua watu bado wanataka dozi, kuanzia sasa tunaenda kupiga kichwani tu.
“Hiyo ndio slogan yetu, Tukipiga kichwani tunacheza na ufahamu. Mwaka huu ni kichwa tu, tumeweka kabisa nyundo kwa ajili ya wale wanaokaza fuvu” Ally Kamwe .