NAIROBI: JKT Queens imeanza vyema michuano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake kanda ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) baada ya kuichapa JKU ya Zanzibar mabao 5-0 leo.
Jamila Rajabu alifunga mabao matatu ‘hatrick’ dakika ya 17, 36 na 71 katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Ulinzi Nairobi nchini Kenya.
Mabao mengine yalifungwa na Winfrida Gerald na Asha Mlangwa dakika ya 27 na 88. Ushindi huo umeonesha mwanga kwa JKT Queens ya kusonga mbele kwani amebakisha mchezo mmoja wa hatua ya makundi.
Kuna makundi matatu na kila kundu kuna timu tatu. JKT Queens itacheza mchezo mwingine Septemba 11 dhidi ya YEI JS ya Sudan Kusini huku JKU ikitarajiwa kucheza dhidi ya YEI Septemba 8, mwaka huu.
Michuano hiyo inatarajiwa kumalizika Septemba 16, mwaka huu ambapo bingwa atawakilisha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
The post JKT Queens yaichapa JKU 5-0 first appeared on SpotiLEO.