DAR ES SALAAM: PENGINE hadi leo huenda wengi wamekuwa wakijiuliza ni nini hasa kilichosababisha kuachana kwa mrembo Paulah Kajala Masanja na msanii nyota wa Bongo Fleva, Raymond Shaban maarufu kama Rayvanny.
Kupitia maelezo yake, Paulah amefunguka kuwa sababu kubwa ya kuvunjika kwa uhusiano wao ni tabia ya Rayvanny kutokuwa na msimamo wa kudumu na mwanamke mmoja.
“Rayvanny alikuwa kwa Fahyma, akaja kwangu, mara akaonekana yupo na Feza, sasa hivi tena amerudi kwa Fahyma. Kwa hiyo msishangae kesho yupo na mtu mwingine.
“Yani yeye kina mtu twende, kitu cha msingi kwake ni kiki na atrend twende,” amesema Paulah Kajala.
Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa mitandaoni, hasa kwa mashabiki wa muziki na wale waliokuwa wakiuona uhusiano wa wawili hao kama mfano wa kuigwa.
Ikumbukwe Rayvanny na Fayma wamebahatika kupata mtoto wao Jaydan na wamekuwa wakiwa pamoja na kuachana mara kwa mara na kubaki wazazi.
Japo kwa sasa inasemekana Fayvany na Rayvanny wameachana tena baada ya Fayvanny kufuta picha akiwa na baba mtoto wake.
The post Kilichowaachanisha Paulah na Rayvanny chafichuka first appeared on SpotiLEO.