Pep Guardiola amepinga madai ya kocha wa Liverpool Arne Slot kwamba mchezaji wake mpya Alexander Isak ya kwamba ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani, huku akisema anamuweka mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland juu kidogo ya Isak.
Guardiola aliongea hayo jana Ijumaa alipokuwa akijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua mtazamo wake kwenye kuwalinganisha Haaland dhidi ya Isak.
“Isak ni mchezaji wa kipekee lakini ukiniuliza kuhusu Haaland naona yuko juu kidogo ya Isak” alisema kocha huyo wa kihispania.