Mwanariadha wa Kimataifa kutoka Tanzania Alphonce Simbu ameshinda mbio za riadha za KM 42 za dunia ambazo zimefanyika Jijini Tokyo nchini Japani na kumshinda mpinzani wake Amanol Petros Kutoka Ujerumani kwa tofauti ya sekunde 0.03.
Alphone Simbu ameshinda mbio za dunia kwa kukimbia kwa saa 2:09:48 na kufanikiwa kupata medali ya kwanza ya dhahabu kwa Tanzania katika mashindano ya dunia ya Tokyo 2025.