Dabi ya Maafande iliyowakutanisha Wazee wa mapigo na Mwendo, Mashujaa Fc dhidi ya Wazee wa kipigo cha Kizalendo, JKT Tanzania imemalizika kwa sare ya 1-1 katika dimba la Lake Tanganyika, Kigoma kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara.
Katika mchezo wa mapema, The Purple Nation, Mbeya City wameibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Fountain Gate Fc katika dimba la Tanzanite Kwaraa, Babati.
FT: Mashujaa Fc 1-1 JKT Tanzania
⚽ 79’ Mundhir Vuai
⚽ 87’ Paul Peter
FT: Fountain Gate 0-1 Mbeya City
⚽ 56’ Kyombo