LIVERPOOL: MENEJA wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Liverpool, Arne Slot ameendelea kufunika taarifa juu ya uwezekano wa Alexander Isak kuanza kwenye mechi ya Merseyside derby dhidi ya Everton, akisema usajili wa rekodi ya Uingereza bado hayuko tayari kutokana kukosa maandalizi ya kutosha.
Mshambuliaji huyo wa Sweden alicheza kwa takribani dakika 60 katika mechi ya ushindi wa 3-2 Jumatano dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa ni hatua yake ya kwanza muhimu ndani ya miezi kadhaa ya hivi karibuni.
“Hebu tuone itakavyokuwa. Ninachojua huenda Alex alihisi wepesi kidogo kwenye mwili wake baada ya dakika 60 alizocheza, ngoja tuone leo atakuwa vipi, halafu mtaonana kikosi kesho.” – Amesema Slot
Slot pia alizungumzia uwezekano wa kumuunganisha Isak na Mshambuliaji mwenzake Hugo Ekitike kwenye safu yake ya ushambuliaji, hatua ambayo inaweza kuwafanya kuwa na safu kali zaidi ya ushambuliaji kwenye ligi hiyo.
I
“Ikiwa wote wawili wako katika utimamu unaweza kuanza kufikiria kuwachezesha pamoja. Ni wazi kabisa kwamba tuna muundo fulani wa mfumo wa 4-3-3, lakini lazima niseme kwamba kuna wakati ni ngumu kuwa na namba 9 wawili .” – ameongeza
Liverpool ndio timu pekee ya Premier League iliyoanza Ligi kwa rekodi nzuri, ikiwa kileleni kwa kushinda mechi zao zote nne za ligi hadi sasa, huku Everton ikiwa ya sita.
The post Slot aendelea kumficha Isak first appeared on SpotiLEO.