MANCHESTER: MENEJA wa Chelsea, Enzo Maresca anakabiliwa na kibarua kigumu cha kumaliza ukame wa miaka 12 bila ushindi kwenye EPL katika uwanja wa Old Trafford wakati timu yake itakapo kuwa wageni wa Manchester United, huku Muitaliano huyo akisisitiza kuwa hakuna wakati mzuri wa kucheza nao licha ya mwanzo wao mbaya wa msimu.
Chelsea haijaonja Ladha ya ushindi dhidi ya United kwenye EPL tangu Juan Mata alipofunga bao la ushindi mwishoni mwa mwezi Mei 2013, huku mechi kati yao ikiwa na historia ya kipekee ya sare nyingi zaidi katika historia ya Premier League ikiwa na sare ya 27.
Chelsea walio katika nafasi ya tano na matumaini ya kuendeleza mwanzo mzuri wa ligi wakiwa hawajafungwa katika mechi nne za Ligi, watawavaa United katika nafasi ya 14 wakiwa na ushindi mmoja lakini Maresca anahofia tishio la vijana hao wa Ruben Amorim ambao wanajipapatua kufuta aibu ya kichapo cha 3-0 kwenye mchezo wa derby wikendi iliyopita.
“Siku zote ni vigumu kucheza na United Old Trafford. Sio sasa, mwaka ujao au mwaka jana, huwa ni vigumu mara zote”
“Baadhi ya michezo waliyocheza msimu huu haina matokeo halisi, hata mchezo wa Man City, hadi 1-0, 2-0 walikuwa mchezoni, 0-0 walipata nafasi chache za kufunga hapana shaka, utakuwa mchezo mgumu”.
“Unapokumbana na hali mbaya, huwa kuna hamu ya kushinda mchezo unaofuata. Mchezo wenyewe ni Dhidi ya Chelsea, nyumbani, mbele ya mashabiki wao, zote ni sababu kwa nini mchezo huu ni muhimu kwao.” – Maresca aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mchezo huo wa Jumamosi.
Mchezaji mmoja wa Chelsea anayeifahamu vyema Old Trafford ni Alejandro Garnacho na Maresca anasema yuko tayari kuanza baada ya kuingia akitokea benchi katika mechi zao mbili za awali
The post United yamtisha Maresca first appeared on SpotiLEO.