DAR ES SALAAM: MSANII nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, ametoa ushauri kwa vijana ambao bado hawajaoa, akiwataka waache kudharau miili yao na kutumia vibaya rasilimali zao kwa uhusiano usio na tija.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Diamond aliandika:
“Kuidharau miili yenu na kupoteza pesa zenu kwa wanawake tofauti hakutawapeleka popote maishani. Sijui ni lini mtakuwa na hekima.
“Jipatie msichana mmoja, au wawili na utulie, kiwango cha juu kabisa watatu, na kama unapitia changamoto nyingi, basi wanne ni sawa.”
Amesema anaamini ushauri huo unaweza kuwasaidia vijana na hata wasanii wenzake kubadili mienendo yao, akisisitiza kuwa yeye ni kioo cha jamii na kauli zake zinapaswa kuwa somo kwa wengi.
The post Diamond: vijana acheni kudharau miili yenu first appeared on SpotiLEO.