DAR ES SALAAM: KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu.
Mirambo anachukua mikoba ya Kidao Wilfred ambaye mkataba wake unamalizika Septemba 30, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wake Cliford Ndimbo, uteuzi wa Mirambo ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo utaanza rasmi Oktoba mosi mwaka huu.
Kidao amedumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017.
Kuondoka kwa Kidao kunatafsiriwa huenda TFF inatimiza yale masharti Matano ya klabu ya Yanga iliyotoa Juni mwaka huu.
Miongoni mwa masharti hayo ilimtaka Kidao ajiuzulu baada ya kutoridhishwa na maamuzi yake.
The post Mirambo akabidhiwa mikoba ya Kidao first appeared on SpotiLEO.