DAR ES SALAAM:
SERIKALI imetangaza kuwapongeza wachezaji waliofanya vizuri hivi karibuni katika mashindano tofauti katika tukio litakalofanyika Jumamosi ya wiki hii.
Akizungumza leo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema miongoni mwa wachezaji watakaopongezwa ni mwanariadha Alphonce Simbu, ambaye ameshinda medali ya dhahabu ya marathon kule Tokyo Japan.
“Simbu alipata ushindi ulioipatia heshima kubwa nchi yetu, huu ni ushindi wa kwanza Tanzania inaupata kupata medali ya dhahabu,”alisema.
Alisema pia, wataipongeza JKT Queens ambao wamekuwa mabingwa wa mashindano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Na Tembo Warriors ambao wamekuwa washindi wa pili wa Cecafa katika mashindano ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika nchini Burundi hivi karibuni.
“Tumeona tuwatie moyo ili kufanya vizuri zaidi kuwapa hamasa na wengine wajitokeze na kuipeperusha bendera ya Tanzania,”alisema.
The post Serikali kuwatunza Simbu, JKT Queens first appeared on SpotiLEO.