Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza Thomas Tuchel ametangaza kikosi cha wachezaji kitakachoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Wales na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Latvia Octoba 14.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 24 Tuchel hajawajumuisha nyota Jack Grealish, Jude Bellingham na Phil Foden huku akiweka wazi kuwa ni kwa kuzingatia mbinu za mechi na ratiba za wachezaji na kusema bado wana nafasi ya kurejea katika mechi zijazo.