DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee, amefichua ushauri wa thamani aliowahi kupewa na mama yake kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto na maadui maishani.
Vanessa amesema kulikuwa na jambo lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu na kumkosesha amani, hali iliyomfanya amtafute mama yake mara kwa mara kuomba ushauri.
“Kuna jambo lilikuwa linanitatiza kweli, linajirudia mara kwa mara kwenye maisha yangu.
Nilikuwa napata matatizo na kukosa amani, nikawa namwambia mama yangu kila mara, ‘mama unajua kitu hiki na hiki…’ nikiwa nashare nae kama mtoto,” ameema Vanessa.
Amesema ushauri ameoupata kutoka kwa mama yake ulimfungua macho na kumsaidia kuelewa namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
“Mara ya mwisho mama akaniambia, ‘Inabidi ufahamu kwamba adui akishajua hili jambo linakusumbua, atakuwa anarudia pale pale.’
Maneno hayo yamenifundisha kuwa si kila maumivu au mapambano lazima uyaseme kuna nguvu kubwa kwenye utulivu,” ameongeza Vanessa Mdee.
The post Vanessa Mdee: Mama alinifundisha siri ya kukabili maadui first appeared on SpotiLEO.