Ni jioni ya soka barani Afrika. Vumbi la kufuzu Kombe la Dunia linaendelea kutimua hewa kwenye viwanja mbalimbali, na kila taifa lina kiu ya kuelekea Marekani, Kanada na Mexico mwaka 2026. Lakini nje ya viwanja, kuna vita nyingine, vita ya ushindi kwenye dau, na hapo ndipo Meridianbet wanaingia vitani, wakiwa na odds kubwa zinazovutia.
Wakati jua likizidi kuungua juu ya ardhi ya Juba, mashabiki wa Sudani Kusini wamejazana uwanjani wakiwa na matumaini makubwa dhidi ya Togo. Huu ni mchezo wa fahari, mchezo wa historia. Togo nao wamewasili wakiwa na lengo moja, pointi tatu. Kwa upande wa Meridianbet, odds zimepambwa vyema, kila upande una nafasi ya kuleta ushindi mzito kwa mbashiri mwenye jicho la kiufundi.
Kwenye Kundi C, moto unawaka tena. Lesotho na Zimbabwe wanakutana katika mchezo wa kukata na shoka. Lesotho wanatamba kwa kuwa na vijana wenye kasi. Zimbabwe, wakiwa na nyota wanaocheza soka la kimataifa kwenye nchi mbalimbali hivyo wanakuja na uzoefu na nidhamu ya kiufundi. Kwa mbashiri makini, mchezo huu una ladha ya pesa, Odds ni kubwa.
Wakati mechi zikisubiri kipenga, kwa nini usiweke dau lako kwenye michezo ya kasino ya Meridianbet? Aviator, Roulette, Poker, Keno, na Superheli zipo hewani na kila mchezo ni nafasi ya ushindi wa papo kwa papo. Piga *149*10# au tembelea meridianbet.co.tz
Usiku unapoingia, macho yote yanageukia Kundi la kifo, ni kundi D. Cameroon, wenye mastaa wanaosakata soka Ulaya, wanakabiliana na Angola, timu iliyoapa kuandika ukurasa mpya wa historia. Wakati huo huo, Cape Verde wanachuana na Eswatini, huku Libya wakisaka ushindi muhimu dhidi ya Mauritius. Cameroon wanaonekana kuwa na nguvu, lakini soka halina uhakika na kila kosa ni nafasi ya mwingine kufaidi. Na kwa mbashiri, kila sekunde ni dhahabu.
Saa 10 jioni, Equatorial Guinea watakuwa nyumbani dhidi ya Liberia, wakati Sao Tome & Principe watapambana na Malawi katika mchezo wa kufufua matumaini. Sao Tome bado hawajapata alama yoyote ile kwenye michuano hii, lakini kwa mbashiri mwenye ujasiri, hilo si tatizo, ni nafasi ya kuvuna kwa odds kubwa.
Kileleni mwa kundi, Tunisia wanaongoza kwa alama 22, wakifuatiwa na Namibia wenye 15. Pambano lao litakuwa na mvuke wa fainali siku ya leo ingawa tayari Tunisia amefuzu. Kila dau hapa linaweza kuwa hadithi mpya ya ushindi na Meridianbet ndiyo mchapishaji wa hadithi hiyo.
The post MERIDIANBET YAWAWEKA WABASHIRI ENEO LA USHINDI KWA MECHI ZA LEO…. appeared first on Soka La Bongo.